Katika ulimwengu wa mitindo, mlimbwende kupata nafasi ya kushiriki show ya Victoria’s Secret, ni sawa na muimbaji kupewa nafasi ya kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy.
Kwa mara ya kwanza, mlimbwende wa Tanzania, Herieth Paul ameungana na walimbwende wote maarufu duniani kwenye show hiyo kubwa, iliyopambwa kwa aina yake na kufanyika jijini Paris, Ufaransa.
Aliungana na warembo maarufu wakiwemo Kendall Jenner, Gigi na Bella Hadid, Alessandra Ambrosio, Adriana Lima, Irina Shayk na wengine.
Kwenye show hiyo Lady Gaga, The Weeknd na Bruno Mars walitumbuiza.
Paul, mwenye miaka 20 amekuwa mmoja wa walimbwende hao takriban 30 walioshiriki kwenye show hiyo.