Michezo

Picha: Ibada ya mwisho ya kuuaga mwili wa Ndikumana kabla ya mazishi

Wananchi wa Rwanda pamoja na wapenzi wa soka wa Afrika Mashiriki siku ya jana walipokea kwa mshituko mkubwa kifo cha ghafla cha aliyekuwa kapteni wa timu ya Taifa ya Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye pia alikuwa ni mume wa muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya.

Mwili wa Ndikumana ukiwa umebebwa na wachezaji wa Rayon Sports, ukipelekwa msikitini kwaajili ya dua ya mwisho

Umati mkubwa watu ulijitokeza katika msikiti wa Qaddafi huko Nyamirambo Rwanda kwaajili ya kumuaga mwanasoka huyo mkongwe. Angalia picha.

Mama yake marehemu Ndikumana akilia kwa uchungu.

Ndikumana anadaiwa kufariki muda mchache baada ya kutoka mazoezi akiwa kama kocha wa timu ya Rayon Sports.

Baba yake Ndikumana

Bado ripoti ya madaktari haijatoka kueleza chanzo cha kifo chake.

Umati wa watu ukimsindikiza Ndikumana

Marehemu alikuwa na mtoto mmoja aliyezaa na aliyekuwa mke wake muigizaji wa Tanzania, Irene Uwoyo.

Ni majonzi

 

Source: Newtimes

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents