Burudani

Picha: Joh Makini afanya collabo na rapper number 3 au 2 kwa ubora Afrika Kusini

Ukiambiwa utaje rappers watatu bora kwa sasa nchini Afrika Kusini, huwezi kuacha kuwataja AKA, Cassper Nyovest na K.O.

Rapper K.O. was born Ntokozo Mdluli
K.O

Katika kuonesha kuwa Weusi hawataki kabisa mchezo mwaka huu, Joh Makini ameingia studio kurekodi wimbo na rapper wa kundi maarufu la Afrika Kusini la Teargas, Ntokozo Mdluli maarufu kama K.O.

10932246_396711587174339_686982286_n
Joh Makini na K.O wakiwa studio

Joh Makini ambaye yupo jijini Johannesburg alikoenda pamoja na G-Nako, Vanessa Mdee na Navy Kenzo, amepost picha Instagram akiwa na K.O na kuandika: #Studio_flow with #KO @mrcashtime himself #2KINGS #ARUSHA_MEETS_JOHANNESBURG #2015 #GODENGINEERING #WEUSIMEETSCASHTIME #amonmyway.”

10958353_1571265163132264_1172971559_n
Joh Makini akiwa na mtangazaji wa MTV Base, Nomuzi Mabena

Hivi karibuni K.O alihit na ngoma ‘Caracara’ aliyomshirikisha Kid X.

Pia ameshirikishwa na AKA kwenye hit single yake ‘Run Jozi’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents