Habari

Picha: Kimbunga cha Irma chaharibu Marekani vibaya

Kimbunga cha Irma kinaendelea kulitesa bara la Amerika. Kimbunga hiko kimeukumba mji wa Florida nchini Marekani na kusababisha maafa makubwa Jumapili hii.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, limeripoti kuwa kimbunga hicho kilianza kwa kukipiga kisiwa cha Marco kilichopo Magharibi mwa pwani ya Florida ambapo kilikuwa na upepo wa kasi ya kilomita 192 kwa saa.

Nyumba takribani milioni 3.4 katika jimbo hilo zimetajwa kukosa umeme kutokana na miundo mbinu yakee kuharibiwa vibaya na kimbunga hicho huku sehemu za mji wa Miami zimefurika maji.

Taya kimbunga hicho cha Irma kimeharibu sehemu za Caribbean na na kuuwa watu wapatao 28 wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents