Habari

Picha: Kongamano la ‘Her Initiative’ lafanyika UDSM

Leo Jumamosi, Mei 14 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) limefanyika kongamano la ‘Her Initiative’ linalosaidia kuwaelimisha watoto wa kike kujitambua na kuishi bila kutegemea watu wengine.

IMG_6367
Ruge Mutahaba wa kwanza kushoto, Jennifer Shigoli wa katikati na Aika wa kundi la Navy Kenzo

Kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya HER INITIATIVE lilihudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam na wasichana wajasiriamali pamoja na wageni kadhaa wakiwemo, Ruge Mutahaba, Le Mutuz, Jennifer Shigoli, Maznat Sinare, Aika na Mhe Bona Kaluwa.

Akiongea na watu waliohudhuria kwenye kongamano hilo, Maza Sinare ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Maznat Bridal alisema aliwahi kuvaa nguo moja kwa miaka saba kwa kuwa kipindi hicho hakuwa na hela lakini alijituma kwa kufanya kazi kwa bidii kwenye ajira yake aliyoanzanayo ya kuuza mitumba bila ya kutegemea mtu wala mwanaume yeyote mpaka kufikia leo anamiliki kampuni kubwa na kupata safari nyingi za kwenda nje na kununua nguo azitakazo.

IMG_6373

IMG_6398
Maza Sinare akiongea na watu waliohudhuria kwenye kongamano hilo

“Siyo muda wote mnakuwa mnaachia miguu mkiendekeza sana ile inachosha na unazeeka mapema. Fanya kazi kwa bidii hata kama biashara yako ni ndogo ila msisahau kujiwekea akiba kwa kufungua mifuko ya kuweka akiba fedha zako hata kama ni kidogo unauza mahindi hutaweza amini siku ukienda unapotaka kuzichukua,” aliongezea.

IMG_6479
Jennifer Shigoli akitoa neno kwenye kongamano la ‘Her Initiative’

Naye Jennifer Shigoli ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investments alisema, “nilipomaliza chuo nilifanikiwa kupata kazi kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali. Nilifanya kazi pale kwa miezi mitatu tu nikawaambia nyumbani naacha kazi nataka kujiajiri, walinishangaa.”

“Nilijiunga na Chuo cha Veta nikajifunza kutengeneza sabuni, baada ya muda nikafungua kampuni yangu ya manufacturing,” aliongeza.

IMG_6529
Aika wa kwanza kulia akiwatambulisha wasanii wao wapya kwenye lebo ya The Industry

Hata hivyo, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Aika alipata nafasi ya kuongea na kusema, “Usiige maisha ya Aika kwenye video, mimi nimelelewa maisha mazuri. Unavyoniona jukwaani tofauti na ninavyoishi maana wasichana wengi wanaishi kutokana na maisha ya kuiga.”

IMG_6536
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bona Kaluwa aiongea na watu waliohudhuria kwenye kongamano hilo

Aidha mgeni rasmi wa kongamano hilo Mhe Bona Kaluwa aliwataka watoto wa kike wasikate tamaa kwani kila kazi ina changamoto zake, hata yeye amepitia changamoto nyingi mpaka kufikia ngazi ya kuwa mbunge wa kuchaguliwa na wananchi tena ukiangalia uchaguzi wa mwaka jana ulivyokuwa mgumu na alikuwa anashindana na wanaume na akafanikiwa kuwashinda.

Tazama picha zaidi.

IMG_6412

IMG_6493
Wageni wakisikiliza maneno yanayotolewa na watoa mada kwenye kongamano hilo

IMG_6468

IMG_6437
Lydia Charles ambaye ni Mwenyekiti wa Her Initiative akitoa neno kwa wageni

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents