Burudani

Picha: Muongozaji wa filamu wa Tanzania ashinda tuzo za Marekani na kuwashangaza kwa ubora wa filamu zake

Pamoja na wengi kuamini kuwa ubora wa filamu za Tanzania ni mdogo, wapo vijana wanaofanya filamu tofauti zinazowashangaza hadi wataalam wa industry hiyo nchini Marekani.

f028eb67-0592-4b8c-a5cb-0aa3e8be12b1
Timoth Conrad akiwa na tuzo aliyoshinda hivi karibuni nchini Marekani

Mmoja wa vijana hao ni Timoth Conrad Kachumia ambaye mwezi huu alishinda tuzo kwenye tamasha la Silicon Valley African Film [Festival] lililofanyika nchini Marekani.

f0d7ee1a-99af-4f9b-bb7b-517086f6632f
Conrad akikabidhiwa tuzo yake

Conrad alishinda tuzo kupitia filamu yake iitwayo Single Zero.

“Ninayofuraha kuwajulisha kuwa filamu yetu ya Single Zero imeshinda tuzo hapa Marekani kwenye tuzo za Silicon Valley African Film Festival, kipengele cha Achievement in Narrative Feature Film,” ameandika Conrad kwenye Facebook.

e1f56fbf-604b-4f54-96a4-a81803201b22
Conrad akiwa na washindi wengi wa tuzo hizo

“Kwenye hicho kipengele nilikua nashindana na Ghana, South Africa, Nigeria. Huu ni wakati wa Watanzania kuamka na kufanya kazi nyingi nzuri zaidi. Huu ushindi sio kitu kidogo upinzani ulikua mkubwa,” ameongeza.

131675f2-b0e3-480f-a657-e711f423114a
Conrad akishukuru baada ya kushinda tuzo

“Asante wanzania wenzangu wote tunaopeana sapoti kulipeleka taifa mbele zaidi, nawapenda sana tupo pamoja.”

Uwezo wa Conrad uliwashangaza watengezaji wa filamu wa mataifa mengine waliokuwa kwenye tamasha hilo na wamempa jina la utani ‘President of Tanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents