Habari

Picha: Rais Magufuli atuma salamu kwa Benjamin Netanyahu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Lieberman Ikulu Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Rais Magufuli ametaka makubaliano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanza mara moja.

“Tanzania na Israel ni marafiki wa miaka mingi, nataka kuona urafiki wetu unakuwa zaidi, nawakaribisha wawekezaji kutoka Israel kuja kuwekeza katika kilimo, madini na gesi na pia kuwepo ndege za moja kwa moja kutoka Israel hadi Dar es Salaam na Kilimanjaro ili kukuza utalii,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amemuomba Mhe. Lieberman kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel, Mhe. Benjamani Netanyahu wa kumualika kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi hapa nchini badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman wa kwanza (kushoto kwake) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wa nne kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florence Turuka wa kwanza kushoto aliyesimama mstari wa nyuma pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents