Aisee DSTV!
SwahiliFix

Picha/Video: Mtanzania Emanuel Austin alivyowapagawisha Wajerumani na tamasha lake

Mtanzania Emanuel Austin ambaye ni mwalimu wa dansi (Choreographer) nchini Ujerumani ameendelea kufanya matamasha yake ambayo yamezidi kufanya vizuri.

Wikiendi iliyopita Austin ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, amefanya tamasha ambalo liliwakutanisha watu takribani 1000 pamoja na wanafunzi kutoka chuo chake cha dansi cha Tanzschule Weiss anachomiliki na mkewe Larissa Bertsch kilichopo katika mji wa Frankfurt.

Tamasha hilo limefanyika kwenye ukumbi wa Abschlussball. Akiongea na Bongo5, mwalimu huyo amesema tamasha hilo lilikuwa dogo waliloliandaa kwa ajili ya kuwakutanisha watu wao wa karibu na wanafunzi kwa pamoja tofauti na matamasha makubwa matatu ambayo wamewahi kuyaandaa na kukusanya watu zaidi ya 11000.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW