HabariPicha

Picha: Waziri Mkuu amwakilisha Rais Magufuli kuaga miili ya askari 14 waliouawa DRC

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 waliouawa nchini DRC katika operesheni ya ulinzi na amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN).

Shughuli ya kuaga askari hao imefanyika kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo.

Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari yao.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wafiwa baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo.

Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents