Michezo

Pogba afunguka kuhusiana na mchezo wa Manchester United dhidi ya Chelsea pia ammwagia sifa Hazard

Pogba afunguka kuhusiana na mchezo wa Manchester United dhidi ya Chelsea pia ammwagia sifa Hazard

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Labille Pogba amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Chelsea ambao utachezwa mapema kabisa majira ya saa nane mchana kwa saa za afrika mashariki.

Kiungo huyo Mfaransa ameongea hayo wakati anaongea na skysport huku akifunguka pia kuhusiana na ukaribu wake na kocha wake Mreno Jose Mouriho.Mchezo huo unavuta hisia za wapenda soka wengi sana licha ya timu hiyo kuonekana kutokuanza vizuri ligi msimu huu,huku wapinzani wao Chelsea wakianza vizuri ligi wakiwa na alama 20 na wako nafasi ya pili wakati United wao wana alama 13 na wakaiwa nafasi ya 8.

Pogba amesema:- “Kwamimi huu ni mchezo bora ambao unatakiwa kuucheza kwa sababu unacheza dhidi ya wachezaji bora, dhidi ya timu bora, na pia dhidi ya stori kubwa”

“Unaweza ukaona jinsi Chelsea walivyoanza ligi vizuri,wameanza kwa ushindi,wanamoja ya mchezaji bora kabisa ambaye kila mtu anapenda kumuona Eden Hazard na wanasema yuko moto kwa upande wangu huyu ndio mchezaji bora wa PL”

“Kwa ujumla mchezo huu utakuwa mgumu sana,tunachezea ugenini na unajua tunacheza na Chelsea kwahiyo itakuwa ni miongoni mwa michezo mikubwa sana”

Pogba amefunguka hayo huku akiwa na wasiwasi juu ya mashabiki wa Chelsea katika dimba la Stamford Bridge na kusema :-

“Kiukweli nata kuongelea hii pointi , Unajua uwanja wa Old Trafford unatusaidia sana kwa sababu unakuwaga wa moto sana,huwaga tunawasikia mashabiki wakitusukuma sana huwaga ni nzuri sana ilakatika mchezo huu wachezaji 12 ndio watakao tusuma na kutubeba tushinde mchezo huo”

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents