Burudani

Posti ya Harmonize aliyomuweka Harmorapa na Harmo Junior mtandaoni yamchanganya msanii mkubwa barani Afrika

Leo moja ya vitu vinavyo-trend zaidi kwenye mitandao ya kijamii hapa Tanzania ni posti ya Msanii wa Muziki, Harmonize kutoka WCB aliyoiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amewaweka wasanii wawili ambao wamefanana naye kimuonekano, Harmorapa na Harmo Junior .

Image result for harmonize
Harmonize

Picha hiyo ambayo amewaweka wasanii wawili ambao amefanana nao kiukweli Harmorapa na Harmo Junior imemchanganya msanii wa muziki kutoka Uganda, Eddy Kenzo ambaye yeye amemuuliza Harmonize kuwa ni picha zake za miaka ya nyuma?

“eddykenzo is this you in 2010??” lakini Harmonize alimjibu Eddy Kenzo kwa kuweka emoji ya kucheka  “harmonize_tz@eddykenzo 🤣🤣🤣”.

Hata hivyo, Posti hiyo ya Harmonize imepongezwa na Mastaa kibao akiwemo Profesa Jay, Bilnass, Zari, Mbosso na Rayvanny.

Posti hiyo ndefu ya Harmonize amemuomba Harmorapa na Harmo Junior kutokata tamaa kwa kile wanachokifanya kwani kila mtu ana ndoto yake.

Harmonize_tz -Mwiko kukata Tamaa ama kukatishwa na mtu yeyote yule katika safari yako ya mafanikio hii safari ni ndefu sana….!!! Utakutana na changamoto nyingi mno….!!! yakiwemo matusi, dharau, uonevu, chuki,
namengine kibao ila pale utakapokubali kukata tamaa ama kukatishwa utakuwa umewavunja moyo watu wengi sana….!!!! (1) familia yako (2) ndugu jamaa na marafiki( 3) hata wale wachache waliokuwa wanakutia Moyo na motisha uongeze jitihada nawengine wengi mno….!!! Itakuwa umewavunja moyo …!! lakini pia M/mungu ni waajabu na hajawahi kukosea katika hii Dunia kila alifanyalo lina maana
Kubwa sana..!!! Wenda kawaumbe Binadam wengine kwa mfano wako nikiwa namaana mnafanana ambalo ni jambo la heri na baraka 🙏 so ukikata tamaa nao pia utakuwa umewaangusha jitihadazako, maarifa, kuzishinda changamoto ndio njia peke inaweza kuleta faraja kwa wengi wanao kuzunguka zingatia hili 👉 #MaishaNiKombolela….!!! God bless my twins brothers 🙏🙏

Related Articles

6 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents