Michezo

Prandelli atangazwa kuwa kocha mpya wa Valencia

Klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu ya soka ya La Liga nchini Uhispania imemteuwa Cesare Prandelli kuwa kocha wake mpya kwa makubaliano ya miaka 2.

prandelli

Mara ya kwanza klabu ya Valencia ilitoa maelezo kwamba Prandelli alitia saini mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka 2017-2018.

Kocha Prandelli alikuwa pamoja na rais wa Valencia Lay Hoon Chan, wakikufuatilia mechi iliyochezwa jumapili hii kati ya Valencia na Atletico Madrid katika uwanja wao wa Mestalla ambapo mechi hiyo uliisha kwa Valencia 0-2 Atletico Madrid .

Prandelli ataanza rasmi kazi kama kocha wa Valencia siku ya Jumatatu tarehe 3 Oktoba na kukinoa kikosi chake.

Prandelli mwenye umri wa miaka 59 aliwahi kufunza timu ya taifa ya Italia kati ya mwaka 2010-2014 na kuifikisha kwenye fainali ya Euro 2012.

Aliwahi kufanya kazi na vilabu vya Galatasaray ya Uturuki msimu wa mwaka 2014-2015 na kupigwa kalamu miezi 5 baadaye kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents