BurudaniHabari

Professor Jay aonyesha thamani ya mashabiki

Professor Jay akiangusha Tsunami mjini Berlin Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Professor Jay, alifanya show ya nguvu mjini Berlin jumamosi tarehe 20 Mei.

Professor Jay akiangusha Tsunami mjini Berlin
Professor Jay akiangusha Tsunami mjini Berlin

 

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Professor Jay, alifanya show ya nguvu mjini Berlin jumamosi tarehe 20 Mei.

Msanii huyu ambaye yupo katika ziara yake ya ulaya, ambayo yeye mwenyewe anaiita ziara ya kutanua soko lake, kujitangaza na kujifunza kama kawaida yake alikonga vilivyo nyoyo za mashabiki walioudhuria.

Dosari pekee iliyotokea katika onyesho ya jana ni maudhurio hafifu ya mashabiki wa mjini Berlin, tofauti na matamasha yake mengine aliyoyafanya hapo awali katika sehemu mbali mbali za ualaya.

Sababu kubwa iliyopelekea maudhurio kuwa madogo mjini Berlin ni mvua kubwa zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo mjini humo na kufanya watu wengi kujifungia majumbani kwao. Sababu zingine ndogo ndogo zimechangia pia.

Pamoja na dosari hiyo msanii Professor Jay hakufa moyo bali alionyesha kuheshimu kila mmoja na kuthamini umuhimu wa kila shabiki pale alipowaangushia tsunami ya nyimbo zake zote tangu enzi za “Chemsha Bongo” mpaka “Nikusaidiaje?” kwa muda wa masaa mawili mfululizo, na kuwachengua vilivyo mashabiki wake hao walioudhuria tamasha hilo.

Professor Jay pamoja na Mambo Jambo Entertainment wanapenda kuwashukuru One World One Love Foundation, Bw. Mganga, Bw. Tom, DJ Frost na mashabiki wote walioudhuria na wasioudhuria tamasha hilo kwa ushirikiano, upendo na kwa kazi kubwa waliyofanya na wanayofanya ya kunyanyua na kutangaza muziki wa kizazi kipya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents