BurudaniDiamond Platnumz

Professor azungumzia Diamond kukosa tuzo MTV, na ujio wa video ya ‘Kipi sijasikia’

Msanii mkongwe wa Hip Hop Professor Jay amesema kuwa kushindwa kwa Diamond kuchukuwa tuzo za MTV kusimvunje moyo kwakuwa alikuwa anashindana na wasanii wakubwa sana Africa.
Professor-Jay1-copy-800x596

Akizungumza na bongo5 leo ,Professor Jay amesema kuwa nafasi aliyopata Diamond na kushindana na wasanii hayo ni ushindi mkubwa wake.

“Diamond lazima ajue katika mashindano kuna kushinda na kushindwa, Kitu ambacho ninaweza kumwambia Diamond asikate tamaa, ameshindanishwa na wasanii wakubwa sana ambao pia ni advantage kwake ,msanii kama Davido pamoja na kufanya muziki mzuri tutambue kuwa nyuma yake kuna Wanageria zaidi ya milioni 150, ambao kiukweli wenzetu wameamka sana kuchangia kuwa support wasanii wao, sisi Watanzania tumekuwa tunazungumza kwa maneno mengi kulipo vitendo ,so mtu kama Davido ameshinda kwa kupigiwa kura na watu wake wengi na muziki wake umefika afrika nzima . Kwaiyo kushindwa kwake Diamond asichukulie kukata tamaa ,yeye achukulie kama changamoto na kuwashawishi Watanzania na mashabiki wake kuendelea ku support muziki wake ili afike mbali zaidi , naamini kuna kila dalili kwa Diamond kuendelea kufanya vizuri zaidi hapo mbeleni, pia nataka niwaambie Watanzania kwamba mtu anapoiwakilisha Tanzania tujitaidi kuweka tofauti zetu nyuma na kum,support wasanii wetu kwa sababu ushindi wake ni mafanikio makubwa ya muziki wetu,wasanii na wetu, na taifa kwa ujumla” Alisema Professor Jay.

Katika hatua nyingine Proffesor Jay amesema kuwa kesho anaingia mzigoni kuanza kushoot video ya ‘Kipi Sijasikia’

“Kesho naanza ku,shoot video ya Kipi Sijasikia, kilichotokea nilikuwa namsubiri tu Diamond, kwa sababu ratiba yake ilikuwa imebana sana, kila kitu sasa hivi kipo set, na tunafanya na Adam Juma, kilichotufanya tu delay kidogo ni kwa sababu alikuwa ameagiza Red na vitu vingine, kwaiyo vikawa vimechelewa kidogo lakini baada ya kuingia vyombo vyake, kesho tunaanza lakini atujajua tutamaliza lini. Adam amenivutia sana sasa hivi kwa sababu ya kubadilisha kamera , Adam ana skills kubwa ya kutumia kamera , lakini kamera ambazo alikuwa akitumia mwanzo zilikuwa zinambana kidogo lakini sasa hivi kwa kuleta kamera hiyo Red na vitu vingine kama hivyo tunategemea uwezo wake anaweza akaonyesha kwa mapana zaidi , na pia tumejaribu tunatumia advantage ya Diamond huko anakozunguka kujaribu kufanya connection, kwa sababu Diamond anaweza kusaidia muziki wetu kifika mbali zaidi”Alisema Professor.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents