Michezo

PSG wametangaza ubingwa wa ligi ya Ufaransa ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya ligi kumalizika

Timu ya Paris St-Germain ambayo inashiriki ligi ya Ufaransa wametangaza ubingwa wa ligi hiyo ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya ligi kumalizika. Baada ya kuifunga timu ya Troyes ambayo inaburuza mkia katika ligi hiyo kwa bao 9-0 huku Zlatan Ibrahimovic akifunga bao nne peke yake.

3227EA3300000578-0-image-a-87_1457910862508

Edinson Cavani, Javier Pastore na Adrien Rabiot kila mmoja alifunga na kuipa PSG magoli 3-0 ya kuongoza ndani ya dakika 19 nza kwanza kabla ya Ibrahimovic kupiga bao tatu ndani ya dakika 10 za kipindi cha pili.

PSG-bingwa

Wamefanikiwa kutangazwa mabingwa mapema kabisa huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja pekee katika mechi 30 za ligi walizocheza, walipoteza kwa kufungwa bao 2-1 dhidi ya Lyon mwezi February. PGS wana wastani wa magoli 62 ya kufunga na kufungwa wakiwa wameruhusu nyavu zao kucheza mara 15.

PSG-bingwa-2

Wameshinda mechi 24 kati ya 30 wakati huo Ibrahimovic akiwa amefunga magoli 31 kwenye mechi 25 alizocheza akifuatiwa na Cavan mwenye magoli 16 katika mechi 27.

PSG-bingwa-1

Vijana na Laurent Blanc wanachukua ubingwa kwa mara ya nne mfululizo kwa style ya aina yake baada ya ushindi mzito wa kihistoria kwenye mechi yao ya ugenini kwa kuifunga Troyes magoli 9-0.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents