Q-Chief Awatolea Uvivu

Q-Chief Awatolea Uvivu
Baaada ya kusemwa sana
kwamba ameoa mwanamke kutoka Kenya aliyemzidi umri wa miaka kumi, Q-Chief
awatolea uvivu watu wote wanaomfuatilia maisha yake na kusema yeye hajali hilo
kwakuwa mapenzi hayachagui na ana uhuru wa kupenda mwanamke kutoka taifa lolote
alitakalo

"Sijazuiwa kupenda mtu hivyo nina uhuru wa kupenda mtu yoyote na kutoka taifa lolote hivyo
wale wanaonisema nimempenda mwanamke wa Kikenya wanajifurahisha midomo"Q-Chief

Q-Chief ameamua kumshirikisha mke wake, ambaye ni mfanya biashara, katika video yake mpya
inayoitwa PAPARAZI.

Video hiyo inawalenga vyombo vya habari, na inamuonyesha Q-Chief na mkewe huyo wakifatiliwafatiliwa
na mpiga picha na akiulizwa maswali kuhusu ndoa yake na shuga mami.

Q-Chief alimuoa mwanamke huyo mwishoni mwa mwaka jana Mombasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents