Burudani

Quick Rocka amtaja aliyemkutanisha na Mimi Mars

Quick Rocka amefunguka na kumtaja mtu aliyemkutanisha na Mimi Mars, mdogo wa mwanamuziki Vanessa Mdee, ambaye amemshirikisha kwenye wimbo wake mpya ‘Down’.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV wiki hii kwamba Jux ndiye aliyemshauri kumshirikisha Mars kwenye wimbo wake huo, ingawa alikua hajawahi kumsikia, kwani ni msanii mpya kabisa kwenye game.

“Unajua wakati naandaa huu wimbo wa ‘Down’ nilikuwa nipo na Jux, na yeye ndio akanishauri kwa nini humu usimuweke Mars? Hapo mimi sijawahi kumsikia kabisa, lakini kwa vile mimi namuamini Jux ni mzuri kwenye uimbaji na ni rafiki yangu nikaamua kumpa Mars nafasi hiyo na yeye kama wimbo unavyousikia hakuchezea bahati,” amesema.

Rocka ameongeza kuwa wimbo huo waliurekodi muda mrefu kidogo kabla hata Mars hajaachia wimbo wake wa kwanza ‘Shuga’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents