Raia wa Australia achoma Bibilia na Qu’ran

Mwanasheria huko nchini Australia amewaacha waumini wa dini ya Kikiristo na Islam katika masikitiko makubwa baada ya kutumia makaratasi ya vitabu hivyo tukufu kusokota na kuvuti Bhangi.

 

Sakata hilo lilionekana YouTube.com ambapo mwanaume huyo amejirekodi akiwa anasokota bhangi kwa kutumia karatasi hizo za vitabu tukufu ili kuangalia ipi inayochoma bora zaidi.

Kanisa la Kikatoliki kimelaani kitendo hicho na pia jumuiya ya Waislamu Australia wamekiri kutokufurahishwa na kuwasihi waislamu watulize hasira.

Mwanasheria huyo alikuwa akifanya kazi katika chuo cha Queensland University of Technology. Msemaji wa chuo alisema kwamba mwanasheria huyu ameshaachishwa kazi na alichokuwa anavuta siyo banghi bali ilikuwa nyasi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents