Habari

Raia wa Burundi adaiwa kuongoza mtandano wa majambazi Tanzania

KIONGOZI wa mtandao wa ujambazi na wenzake sita, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa, kwa kukutwa na bunduki moja aina ya SMG, risasi 50 na magazine mbili.

Na Paulina David, Mwanza

 

 

 

KIONGOZI wa mtandao wa ujambazi na wenzake sita, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa, kwa kukutwa na bunduki moja aina ya SMG, risasi 50 na magazine mbili.

 

 

 

Kiongozi huyo ambaye inadaiwa kuwa mkazi wa Chanuzu nchini Burundi na wenzake, walikamatwa na Polisi wilayani Geita mkoani hapa.

 

 

 

 

 

Wengine waliokamatwa na Polisi ni mkazi wa kati ya Chato na Biharamlo, mkazi wa Nkome Geita, Nyawilimili, Geita, Katoro Geita na Buselesele Geita

 

 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Zelothe Stephen alisema kuwa, watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa majambazi hatari, walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kwamba wengine nane wanaounda mtandao wa ujambazi wilayani humo, wanasakwa na Polisi.

 

 

 

Kwa mujibu wa Stephen, watuhumiwa hao, wamekuwa wakijihusisha na uvamizi wa kutumia silaha, utekaji wa magari katika maeneo ya Geita, Bukombwe Chato na Biharamlo .

 

 

 

Vilevile, polisi wamebaini kuwa, mmoja wa watuhumiwa hao anadaiwa kuwa ndiye anayefuatilia maeneo ya kwenda kuvamia, mwingine ni mtafutaji wa risasi.

 

 

 

Wakati huo huo: Suzy Butondo kutoka Shinyanga anaripoti kuwa, Jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za ujambazi.

 

 

 

Kamanda wa polisi mkoani humo, Ibrahimu Shaibu jana alisema kuwa, watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia kijiji cha Mwabomba wilayani Kahama na kuwapora watu wanne.

 

 

 

Watuhumiwa hao walikamatwa na kutambuliwa na wananchi waliovamiwa kutokana na mmoja wao kukutwa na jeraha la kukatwa mapanga kichwani wakati akipambana na Rocket Charles, walimpora baiskeli.

 

 

 

Alisema wakazi wa kijiji hicho wanaendelea kuwasaka majambazi wengine waliohusika na uvamizi huo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents