Habari

Rais Jacob Zuma awachana wanaotaka kumng’oa madarakani

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amewaita watu wanaofanya maandamano ya kushinikiza kumng’olewa kwenye kiti hicho kuwa ni wabaguzi wa rangi.

Zuma alisema hayo katika kumbukumbu ya Chris Hani Memorial. “The marches that took place last week demonstrated that racism is real. We can’t allow and assist racists to take our country backwards,” amesema Zuma.

Maelfu ya raia wa nchi hiyo pamoja na vyama vya upinzani vimeungana kutaka kumng’oa madarakani rais huyo huku chama kikuu cha wafanyakazi cha COSATU ambacho kinakiunga mkono chama tawala cha ANC kikiyaungana katika maandamano hayo.

Sababu kubwa ya kumtaka Zuma kujiuzulu ni kutokana na ufisadi wa fedha za umma pamoja na kuwa na uhusiano wa karibu na familia moja ya jamii ya wahindi nchini humo ijulikanayo kama Gupta ambayo inadaiwa na nguvu kubwa ya ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Zuma.

Hata hivyo raia Zuma amesema yeye hausiki na hayo yote wanayomtuhumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents