Habari

Rais Magufuli aahidi mazuri kwa wafanyabiashara wa Afrika Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusini kujitokeza na kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ina mazingira bora.

Rais Magufuli ameyasema hayo, Jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini katika mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

“Napenda kuwahakikishia wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza Tanzania kuwa nchi hii ina amani, tangu tupate uhuru mnamo mwaka 1961,ina mazingira mazuri ya kibiashara,utulivu wa kiasiasa pamoja na uchumi unaotabirika hivyo nawasihi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuwekeza nchini kwetu,”alisema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa wamekubaliana na Rais Magufuli kukuza ushirikiano hasa wa kiuchumi wa nchi zote mbili.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents