Habari

Wanajeshi waasi wa Ivory coast waomba msaada

Wanajeshi kutoka nchini Ivory Coast ambao waliasi mwanzoni mwa mwaka huu wamekubali kuachana na maombi yao ya malipo zaidi kutoka serikalini.

Msemaji wa wanajeshi hao walioasi, Sajenti Fofana ameomba msamaha kwa Rais wa nchi hiyo Bw.Alassane Outtara mjini Abuja-Nigeria. Kitendo cha sajenti huyo kuomba msamaha kinaashiria dalili zote za kumaliza mgomo uliokuwepo kati ya waasi hao na serikali.

Waasi hao wa kijeshi ambao wapo maelfu,waliilazimisha serikali ya Ivory Cost kuwapa malipo zaidi ya dola elfu nane kwa kila mmoja wao.Pia katika Mwezi huu wanajeshi hao walipaswa kulipwa malipo mengine.

Wanajeshi waasi waliopo katika mji wa Bouke wamekosoa mpango huo na kusema kuwa hawakushauriwa.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents