16 bora ya ligi ya mabingwa kuanza wikiendi
Hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Afrika inatarajiwa kuanza kutimua vumbi wikiendi hii katika hatua ya makundi, takribani michezo mitano itachezwa siku ya Ijumaa na mbili zikichezwa siku ya Jumamosi na moja kuchezwa Jumapili.
Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Afrika, klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini itaanza kutetea taji lake Jumapili hii wakiwa wenyeji katika mchezo utakao chezwa dhidi ya Ethiopia.
Kocha wa Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane
Kocha wa klabu hiyo, Pitso Mosimane amesema wana hofu ya kutetea taji lao kutokana na timu zote kuwa imara
Mwaka jana walikuwa katika nafasi ya pili katika klabu zenye ushindani nchini Afrika Kusini baada ya ushindi wake wa magoli 3 kwa 1 dhdid ya Zamalek ya Egypt katika mchezo wa fainali.
Mosimane, ambaye alishawahi kucheza Afrika kusini pamoja na kuwa kocha nchini humo amesema ratiba ya timu yake inaweza kuathiri timu yake
BY HAMZA FUMO