Shinda na SIM Account

Rais Magufuli ampa maagizo haya Prof. Kabudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza  Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi kuunda timu zitakazoshughulikia biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi pamoja na migodi mingine ya dhahabu.

Mh. Rais ameyasema hayo baada majadiliano kati ya wataalamu wa Tanzania na wa kampuni ya Barrick Gold Mine kukamilika na  pande zote mbili .

“Nataka machimbo yote ya dhahabu mchakato kama huu ufanyike, pia nakuagiza Prof. Kabudi biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi nako ni lazima kufuate utaratibu huu, asiyetaka aondoke,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo  Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi badala ya baadhi yao kuzibeza kwa kuwa zina manufaa kwa taifa na wananchi wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW