Michezo

Kocha Mtibwa Sugar ampa kiburi Nditi

Klabu ya Mtibwa Sugar chini ya Kocha wao mkuu Zuber Katwila “Puchetino” wana taraji kujitupa uwanjani hapo kesho siku ya Jumamosi kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo namba 55 wa Ligi kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Manungu Arena.

Kuelekea mchezo huo wa Jumamosi wana tam tam dhidi ya Tanzania Prisons kocha, Katwila ameelezea maandalizi yake kupitia mtandao wa timu hiyo.

“Tunamshukuru Allah tunaendelea vizuri na mazoezi na kila mtu katika timu kuanzia wachezaji hadi viongozi wana hali ya kupigania timu naweza kusema hali ni shwari kwa upande wa kambi yetu,” amesema Zuber Katwila.

Pia kocha huyo amesema kiungo na nahodha wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amekuwa akimrahisishia kazi akiwa uwanjani kwakuwa anamkabidhi majukumu mengine.

Nahodha wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi 

“Nditi ni kaptain lakini ni mtu muhimu awapo uwanjani kwakuwa anasaidia sana na ananirahisishia mimi kazi huwa nampatia jukumu la kutoa maelekezo kwa wenzake hivyo akiona hawaendi kama nilivyo elekeza huwa anafanya jukumu hilo haraka kwakuwa yeye yuko karibu nao uwanjani na mimi niko mbali au anaweza pokea maelekezo kutoka katika benchi na kuyapeleka moja kwa moja kwahiyo nadhani kila kocha anatamani kuwa na mchezaji wa kariba ya Nditi.”

Katika michezo mitano iliyopita baina ya timu hizi mbili matokeo yamekuwa ya sare hivyo kila timu ita ingia uwanjani ikitafuta ushindi kwa mara ya kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents