Habari

Rais Mstaafu Mwinyi asifia mradi wa mabasi yaendayo kasi

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameyasifia mabasi ya mwendo kasi baada ya hapo jana kufanya ziara yake ya kutembelea mradi huo ulioanza mwezi May mwaka huu.

13393943_1534104179937328_1239726187191716485_n

Ziara ya Mwinyi ilianzia kituo cha Morocco na kwenda mpaka staendi ya Gerezani, Kariakoo na baadaye alielekea stendi kuu ya Kivukoni kwa kukamilisha ziara yake hiyo. Rais Mwinyi alisema kuwa, “Usafiri huu ni mkombozi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya usafiri unaosababishwa na msongamano wa magari katika maeneo ya mjini.”

Aidha Mwinyi aliongeza kuwa amejionea ujuzi na uroda kama watu wanavyosema na amefurahia sana mazingira ya mabasi hayo kwa sababu yanaubora na hayana usumbufu wala msongamano.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuheshimu njia za mabasi hayo ili kuepusha ajali zisizokuwa za ulazima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents