Habari

Rais Samia: Matumizi ya gesi ni lazima sio anasa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa matumizi ya nishati safi ya gesi ni lazima wala sio anasa kama ambavyo wengi wanafikiri.

Ameyasema hayo leo Mei 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.

Rais Samia amesema ili kuweza kukabiliana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia ni lazima jamii ikabadfilika kifikra na kuanza mara moja kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi.

“Niwatake wananchi wasiwe na hofu kuhusu kutumia nishati ya gesi katika kupika maharage, kusonga ugali wala ladha ya chakula na upatikanaji wa matandu, serikali inatafuta mpango mkakati mzuri wa kutatua hayo yote,” amesema Rais Samia

Aidha amewataka wananchi kuendelea kupanda miti ili kuendelea kutunza mazingira na kufidia uharibifu wa misitru ambao umekwishatokea na kusababisha athari mbalimbali.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents