Habari

Rais wa Bolivia na makamu wake watangaza kujiuzulu, wananchi waingia barabarani na kusherehekea maamuzi yao (+video)

Rais wa Bolivia Evo Morales ametangaza kujiuzulu kupitia hatuba yake na luninga. Uamuzi huo unakuja muda mchache baada ya uchunguzi uliyofanywa na OAS juu ya matokeo ya uchaguzi wake ambao ulitangaza kuwamshindi mwezi uliyopita kugubikwa na udanganyifu.

Evo Morales ametangaza hatua hiyo siku ya Jumapili kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu bungeni baada ya jeshi, polisi na upinzani kumtaka kufanya hivyo.

“Matamanio yetu makubwa ni kuona amani inarejea kwa watu wetu,” amesema Morales katika luninga wakati huo huo makamu wake wa rais Alvaro Garcia Linera naye akitangaza kujiuzulu kwake.

“Ninaomba kuacha kushambuliana, kuacha kuchoma vitu na kushambuliana,” Morales alipowaambia watu wa Bolivian.

Rais huyo amenukuliwa akisema kwamba ameamua kuitisha uchaguzi mwengine ili wananchi wa Bolivia waweze kuchagua serikali mpya kwa njia ya kidemokrasia.

Image result for Bolivia Evo Morales

Kwa wiki kadhaa Bolivia imeshuhudia machafuko na ghasia dhidi ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 20. Watu watatu wameuawa na zaidi ya 300 kujeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi uliopita yalimpa ushindi Morales kwa asilimia 10 dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa. Upande wa upinzani umeishutumu serikali kwa udanganyifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents