Michezo

Rais wa TP Mazembe akubali Samatta ajiunge na KRC Genk ya Ubelgiji

Hatimaye mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.

picsamatta

Mchezaji huyo alitarajia kurejea nchini wiki hii kwa ajili ya safari ya Ubelgiji.

Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki. Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka lake.

Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, ili kucheza soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda huko na alikuwa tayari kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika Aprili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents