Habari

Rais wa Myanmar, Htin Kyaw ajiuzulu

Rais wa nchi ya Myanmar ambayo inapatikana katika bara la Asa, Htin Kyaw amejiuzulu.


Rais Htin Kyaw

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN imesema, taarifa iliyotolewa na serikali yake imesema rais huyo amejiuzulu kutokana na afya mbaya.

Htin Kyaw aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo mwaka 2016 baada ya kushinda uchaguzi uliositisha miaka kibao ya uongozi wa kijeshi.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Myanmar, makamu wa rais Myint Swe atakalia kiti cha Urais kwa muda baada ya kujiuzulu kwa Htin Kyaw.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents