Habari

Rais wa Uturuki aigomea Marekani, adai taifa lake litaendeleza mashambulizi Syria, Urusi yatoa onyo kali

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekataa wito wa Marekani wa kusitisha mapigano kaskazini mwa Syria, akisema kuwa Uturuki itaendelea na mashambulizi yake.

Uturuki

Ameeleza hayo wakati ambao Naibu Waziri wa Marekani, Mike Pence na waziri wa mambo ya nje, Mike Pompeo wakiwa wanajiandaa kuja kufanya makubaliano.

Siku ya Jumanne, nchi ya Urusi  imetoa onyo kuwa haitaruhusu mapigano kutokea tena baina ya majeshi ya Uturuki na Syria.

Uturuki imesema kuwa lengo la kuendelea na mapigano hayo ni kutaka kuwaondoa wanajeshi wa kikurdi katika mipaka. Uturuki inaaminika kuwa wanamgambo wa kikurdi ‘Kurdish-led Syrian Democratic Forces (SDF)’ ni asasi ya kigaidi

Vikosi vya Uturuki pia vimebuni kile ambacho serikali yao inataja kuwa “eneo salama” la kuwapa makazi wakimbizi milioni mbili wa Syria ambao wamepewa hifadhi katika nchi hiyo.

Kujiondoa kwa majeshi ya Marekani katika ukanda huo kulitangazwa wiki iliyopita na kuipa Uturuki mwanya wa kuanza mashambulizi, mkosoaji wa serikai ya Trump alieleza.

Marekani ilirudia kukanusha hilo siku ya jumatatu. Wananchi wengi wameuwawa katika oparesheni hiyo na watu wapatao 160,000 wamekimbia makazi yao, kwa mujibu wa UN.

Rais Erdogan amesema nini?

“Wanataka tuache kupigana ‘. Hatuwezi kusitisha mapigano hayo,” bwana Erdogan aliwaambia waandishi siku ya Jumanne.Turkish President Recep Tayyip Erdogan. Photo: 13 October 2019Rais Erdogan asisitiza kuwa ataendelea na mapigano

” Wanatulazimisha kusitisha mapigano huku wakitangaza kutuwekea vikwazo. Lengo letu liko wazi kabisa. Hatuna hofu na vikwazo vyovyote,” rais Erdogan aliongeza.Map showing control of north-east Syria on 14 October 2019Presentational grey line

Rais Erdogan alikuwa anatarajiwa kukutana na bwana Pence na Pompeo huko Ankara siku ya alhamisi.

Bwana Pence alitoa angalizo kuwa vikwazo ambavyo vimewekwa na Marekani dhidi ya Uturuki vitavuruga mambo. Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akipata msukumo mkubwa sana kutoka kwa washirika wenzie wa Nato wa kutaka Marekani kuchukua hatua dhidi ya Uturuki.

Nini kinaendelea sasa?

Baada ya kufikia makubaliano na vikosi vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi, jeshi la Syria lilianza kufanya mashambulizi kuelea mpakani siku ya Jumatatu.

Vyombo vya habari vya Syria vilitangaza kuwa vikosi vya serikali vimeingia katika mji wa Manbij, eneo ambalo Uturuki inataka kubuni “eneo salama”.

Wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji wanaopinga serikali ya Uturuki walianza kukusanyika karibu na mji huo.

Mkataba huo ulionekana kuimarisha utawala wa rais wa Syria Bashar al-Assad kwani ulimaanisha vikosi vyake vitarejea katika maeneo ya kaskazini mashariki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012, baada ya kujiondoa kwao katika maeneo mengine ili kukabiliana na waasi kutoa nafasi kwa wanamgambo wa Kikurdi kuchukua udhibiti wa eneo hilo.

Image result for Uturuki plane attack syria

Licha ya kupinga jaribio lao la kutaka kujitenga na kujitawala, Bw. Assad hakupigania kukomboa eneo hilo, hasa baada ya wapiganaji wa Kikurdi kuwa washirika wake katika vikosi vya muungano dhidi ya IS kwa ushirikiano na vikosi vya Marekani.

Kando na kupiga vita IS, Wakurdi walikuwa kiungo muhimu kwa Marekani katika hatua ya kudhibiti ushawishi wa mahasimu wao Urusi na Iran katika mzozo wa Syria.

Kwa sasa, vikosi vya Syria havitapelekwa katika miji ya Tal Abyad na Ras al-Ain, ambako Uturuki imeelekeza juhudi zake.

Rais Erdogan wa Uturuki anasisitiza kuwa oparesheni hiyo itaendelea hadi pale inchi hiyo itakapofikia “malengo yake” licha ya kuingiliwa na vikosi vya serikali ya Syria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents