Burudani ya Michezo Live

Rais wa Venezuela asitisha mazungumzo na upinzani kisa Marekani

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameilaumu Marekani kwa vikwazo ilivyoiwekea nchi hiyo na kuamuru wawakilishi wa serikali yake kutosafiri kuelekea Barbados kwa mazungumzo yaliyotarajiwa kufanyika na wanasiasa wa upinzani.

Image result for Venezuela president Nicolas Maduro stop conversation with opposite party because of trump

Taarifa ya serikali ya Venezuela imesema Maduro ameamua kutowatuma maafisa wake kwa mazungumzo hayo yaliyopangwa kufanyika leo siku ya Alhamisi na kesho pamoja na kiongozi wa upinzani Juan Guaido kutokana na uchokozi mkubwa unaoendelezwa na utawala wa rais Trump.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Rais Trump ameagiza kufungiwa kwa mali zote za serikali ya Venezuela zilizoko Marekani na pia amezuia kufanyika kwa biashara ya aina yoyote na uongozi wa nchi hiyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW