Tupo Nawe

Rapper Cardi B atangaza albamu yake ijayo kuita ‘Tiger Woods’ jina la mchezaji Golf, atoa sababu hizi 

Rapper wa kike kutoka nchini Marekani Belcalis Marlenis Almánzar alimaarufu Cardi B, amesema kuwa albamu yake ijayo anafikiria kuipa  jina la mchezaji Golf maarufu duniani, Tiger Woods.

Mshindi huyo wa tuzo za Grammy, Cardi B ameyasema hayo wikiendi hii kupitia ‘Instagram Live’ ikiwa ni maalum kwa mashabiki wake.

Cardi amepanga kufanya hivyo kutokana na kuvutiwa na mapito ya Woods hasa kipindi ambacho alikuwa akisemwa sana huku wengi waliamini kuwa mchezaji huyo bora kabisa wa Golf duniani uwezo wake umekwish ndani ya uwanja na fedha kiujumla.

Lakini Woods aliishangaza dunia baada ya kurejea na ushindi wa kihistoria katika mchezo wa Golf.

‘Everything I’m working on right now is straight to my album,’ she said in the selfie video.

”Kilakitu ninachofanya kwa sasa moja kwa moja kinahusiana na albamu yangu,” amesema Cardi B kupitia akaunti yake ya Instagram.

Cardi B ameongeza kuwa ”Nafikira albamu yangu kuiita ‘Tiger Woods,” amesema mrembo huyo huku akionekana  akirembwa.

Dada huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema anakumbuka namna kila mtu alivyokuwa akimzungumzia vibaya Tiger Woods lakini amerudi na amewadhihirishia watu uwezo wake na kushinda taji kubwa duniani, hivyo ndivyo anavyokwenda kuipa jina albamu yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW