Burudani

Rapper Hennesseyy na mmiliki wa lebo ya Spacious Africa aeleza kuhusu ujio wa ngoma yake mpya

Mmiliki wa lebo ya muziki ya Spacious Africa ambaye pia ni rapper, Hennesseyy amefunguka kuhusu mipango yake ya kuachia nyimbo zake mwenyewe bada ya kushirikishwa kwenye ngoma mbili.

Akiongea na Bongo5, Hennesseyy amesema muda sio mref ataachia wimbo wake mpya ambao ametumia staili ambayo watu hawjawahi kumsikia.

“Umefikia wakati wa mashabiki kunisikia katika nyimbo zangu baada ya kunisikia katika nyimbo za Elly da Bway ikiwemo ‘BOSS’ na ‘SURA’. Kiukweli nimewaandalia vitu vizuri sana na kwa wimbo huu itakuwa ni suprise kwa sababu ni kitu kikubwa sana,” amesema rapper huyo.

“Nakuja na staili ambayo ipo tofauti kidogo na vile ambavyo watu walinisikia na ninauhakika wataipenda kwa sababu ninaamini mashabiki wanapenda kitu kizuri,” ameongeza.

Msanii huyo anatarajia kuanza kushoot video ya wimbo wake huo mpya wiki ijayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents