Michezo

Ratiba ya raundi ya tano ya kombe la FA

Ratiba ya raundi ya tano ya kombe la FA, Chelsea watacheza nyumbani dhidi ya Manchester City, Klabu ya League One Shrewsbury Town, ndo timu ya chini zaidi miongoni mwa timu zilizosalia kwenye shindano hilo nayo itakuwa mwenyeji wa Manchester United katika uwanja wa New Meadow.

MK Dons v Chelsea, 4th round FS cup. pic Andy Hooper/daily mail oscar scores

Arsenal mabingwa watetezi watakutana na Hull, hii itakuwa kama marudio ya fainali ya 2014. Itakuwa mara ya tatu mfululizo kwa klabu hizo mbili kukutana katika dimba hilo.

Meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema mechi kati ya klabu yake na Manchester City ndiyo “mechi kubwa” na itavutia sana mashabiki.

“Hiyo ni fainali tayari!” aliongeza.

Droo kamili:

Chelsea v Manchester City
Reading v West Brom or Peterborough
Watford v Leeds United
Shrewsbury Town v Manchester United
Blackburn v Liverpool or West Ham
Tottenham v Crystal Palace
Arsenal v Hull
Bournemouth v Everton

Mechi zitachezwa wikendi ya 19-22 Februari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents