Burudani

Ray C amzimikia ‘Abdul Haji’ shujaa wa Westgate aliyeokoa watu kibao mikononi mwa magaidi

Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita.

Nairobi_escape_2684620c
Abdul Haji akisaidia baadhi ya watu waliokuwa ndani ya mall hiyo kutoka nje

Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.

87dfd88e1c4411e387c922000aeb0d21_7
Ray C

“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.

“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.

Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”

NAIROBI-GIRL_2684619b
Haji akimuokoa mtoto wa kizungu

Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.

Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.
NAIROBI-POLICE_2684617c
Haji na mwenzake wakipambana na magaidi hao

Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents