Burudani ya Michezo Live

Rich Mavoko: Najiandaa kuachia ngoma mpya ‘soon’

Rich Mavoko si msanii aliyepo kwenye vichwa vya habari kama ilivyo kwa wasanii wengine wa WCB hasa bosi wake, Diamond. Baada ya kuachia hit yake, Kokoro, amekuwa kimya kiasi, na sasa huenda yu mbioni kuuvunja.

Hitmaker huyo ameonjesha picha ya kile kinachoonekana kuwa ni video yake mpya na kuandika: Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ???? #Showme

Nimemtafuta kumuuliza iwapo matukio ya kisiasa yamemfanya awe muoga kuachia wimbo mpya.

“Hapana, siasa ipo kila siku ila now naona wasanii wengi wanaliongelea hilo, ila mie sidhani kama ngoma nzuri inashindwa kwenda kwaajili ya siasa,” amesema.

Kuhusu muda wa kuachia wimbo wake Mavoko amesema, “Wiki hii naweza kufanya hivyo, au wiki ijayo mwanzoni.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW