Shinda na SIM Account

Rick Ross aruhusiwa kutoka hospitali

Rapper Rick Ross ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kukaa hospitali kwa siku nne akipatiwa matibabu.

Bosi huyo wa Maybach Music Group alifikishwa hospitali mjini Florida siku ya Ijumaa baada kupata tatizo la kushindwa kupumua na kupoteza fahamu.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, rapper huyo ameruhusiwa Jumatatu asubuhi kurudi nyumbani lakini bado anaendelea kupata matibabu katika makazi yake.

Mtandao huo umeongeza kuwa Ross alihamishwa katika hospitali mbili tofauti kwa ajili ya kupat matibabu kutokana na hali yake ilivyokuwa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW