Michezo

Ripoti: Ndoa ya David na Victoria Beckham ipo kwenye mawe

David na Victoria Beckham huenda wakawa wanakaribia kupeana talaka baada ya tetesi za muda mrefu kuwa ndoa yao ipo kwenye mawe kuongezeka zaidi.

weddingSUM_1830702b

Wawili hao hivi karibuni walionekana wakibishana kwa sauti za juu kwenye tukio moja kwa mujibu wa jarida la OK!

Ripoti hiyo inadai kuwa wakati wawili hao wanatoka kwenye uzinduzi wa moja ya maduka ya Victoria, walionekana wakirushiana maneno makali hadharani na kuwaacha mashuhuda midomo wazi.

Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun kuwa Victoria amekuwa akifanya kazi nyingi zenye stress kibao huku David akionekana kupumzika zaidi baada ya kustaafu.

Ripoti hiyo inaendelea kudai kuwa ratiba zao za kazi zimezidi kutengeneza ufa kwenye uhusiano wao.

Hafla ya uzinduzi wa Mayfair London ya Victoria inadaiwa kuwa ndio siku pekee wawili hao walionekana pamoja hadharani tangu wiki kadhaa zilizopita na kuongeza zaidi tetesi kuwa hawako sawa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents