Burudani

Rita Ora apata dili la kuwa miongoni mwa wahusika wa movie ya POKÉMON

Msanii Rita Ora ni miongoni mwa wahusika watakao igiza katika movie ya Pokémon lakini jukumu la Ora katika filamu hiyo bado halija wekwa wazi kwa sasa lakini movie hiyo itakuwa cinemas Mei 10, 2019.

The Hollywood Reporter linasema kwamba kwa sasa shooting zimeshaanza kwa ajili ya filamu hiyo. Ora kwa kweli si mgeni kwa sinema, alishawahi kucheza kama dada wa Christian Gray, Mia, katika Fifty Shades Freed.

Kazi za Ora kwenye skrini zitaendelea kuangaza, zaidi ya yote hayo pia Ora ataonekana katika filamu ya kihindi Wonderwell.

Kazi ya kimuziki za Rita bado zinaendelea na kwa sasa anaifanyia kazi albamu yake mpya na mwishoni mwa mwezi huu Ora atatumbuiza katika tuzo za Brit Awards Februari 21.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents