Habari

Aliyeokoa maisha ya Lissu ni mteule wa Rais Magufuli – Waziri Nchemba (+video)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa watu waache kutumia jina la Mhe. Lissu kwenye majukwaa ya kisiasa kama mtaji ile hali hata mtu wa kwanza aliyemsaidia kipindi alivyoshambuliwa kwa risasi na kumpa huduma ya kwanza alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ni mteule wa Rais Magufuli.

Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. mwigulu amesema hayo mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mitunduluni.

Aidha Dkt. Nchemba amesema kuwa kuna vyama vya kisiasa vimekuwa vikitaja jina la Lissu kama mtaji na hawaangalii mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM.

Tazama video hapa chini kumsikiliza Waziri Nchemba akitema cheche.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents