Michezo

Roger Federer aendeleza ubabe dhidi ya Rafael Nadal

Mchezaji wa tenisi,  Roger Federer ameendeleza ubabe kwa kutwaa ubingwa wa Shanghai Masters baada ya kumfunga mchezaji namba moja duniani kwa ubora, Rafael Nadal kwa seti 6-4, 6-3 katika fainali iliyomalizika mchana huu.

Roger Federer

Raia huyo wa Uswisi ametwaa taji lake la sita ndani ya mwaka 2017, akiwa ndiye mchezaji pekee aliyemshinda Nadal kwenye fainali kubwa nne ndani ya mwaka huu.

Federer  (36), alikuwa kwenye kiwango kizuri leo baada ya kumuadhibu Nadal kwa muda wa dakika 72 pekee.

Federer sasa ndio mchezaji pekee ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Nadal kama mchezaji namba moja duniani mwishoni mwa mwaka huu, endapo atafanya vizuri kwenye michuano ya ATP mwezi ujao nchini Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents