Mitindo

Tinga Sneakers zako na gauni tuone!

Offcourse now ni time ya mitindo kutoka Bongo5, hapa utapata habari mbalimbali za mitindo zitakazokupa mwangaza katika ulimwengu huu wa sasa wa kimitindo zaidi. Na leo tutacheki ni namna gani unaweza ukatinga Sneakers (raba) zako huku ukitupia na gauni lako na ukabamba.

Mtindo huu unaweza ukawa unauchukulia poa sana ila ngoja nikuambie kitu, sio wote wanaoweza kuvaa viatu virefu na wakamudu mikiki miki yake hasa kwenye tafrija zilizo na mchanganyiko wa watu wengi.

Kuvaa raba ama Sneakers itakusaidia wewe kuweza kuwa simple and unique katika  event, vile vile hautachosha miguu yako wala kuipa ganzi itakayokufanya ushindwe kutembea.

Kuonyesha kuwa mtindo huu unakuwa kwa kasi tayari mastaa kadha weshatinga muonekano huo, hivyo na wewe ni time yako kujaribu mtindo huu ila kuhakikisha unatinga raba kali na zenye kusimimua  ili uwe topic katika event.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents