Michezo

Roger Federer amchakaza Marin Cilic na kuvunja rekodi

By  | 

Mchezaji maarufu wa Tenesi duniani, Roger Federer ameendeleza ubabe wake kwenye michuano ya wazi ya Wimbledon kwa kumchakaza mpinzani wake Marin Cilic na kuweka rekodi ya kutwaa mataji 8 ya michuano hiyo .

Roger Federer

Roger Federer

Katika mchezo huo wa fainali ambao ulichukua saa 1 na dakika 40, Federer alionekana kuutawala mchezo kwa ushindi wa seti  6-3, 6-1 na 6-4 dhidi Marin Cilic.

Federer amezidi kujikita kileleni kwa kuwa mcheza tenesi mwenye makombe mengi zaidi duniani ( Grand Slam 19) baada ya ushindi wa jana.

Kwa upande wa michuano hiyo, Federer amevunja rekodi ya Bjorn Borg iliyoweka mwaka 1976 ya kushinda mashindano ya Wimblendon bila kupoteza seti hata moja katika mchezo wa fainali.

Wachambuzi wengi wa mchezo wa Tenesi wamesema sababu za Mcroatia Marin Cilic kupoteza mechi hiyo ni kukosa uzoefu kwani hii ilikuwa fainali yake ya kwanza ya mashindano hayo huku ikiwa ya 11 kwa Rodger Federer.

By Godfrey Mgallah

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments