Roma aogopa kujitabiria kifo, ni kutokana anayoandika kutokea kweli

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Roma amesema kutokana na mambo mengi anayoandika katika ngoma zake kutokea kweli muda mwingine hufikia hatua ya kuhofia.

Rapper huyo katika mahojiano na The Playlist, Times Fm amesema baadhi ya matukio kama Rais. John Magufuli kukalia madaraka hayo ni moja ya vitu alivyoandika toka miaka nyuma na kutokea kweli.

“Kuna muda mwenyewe nakaa napitia mistari yangu najitafakari naona mmmh! eeh Mungu vingine ambavyo nimeviandika visije vikatokea kweli, nisije nikaandika nafa kesho halafu walete” amesema.

“Roma kasema anaenda Zimbabwe lakini kitu kilichotokea Zimbabwe ni mfano wa nchi nyingi za Afrika, watu wanatamani kifanyike kitu kama kile” ameongeza.

Kwa sasa Roma anatamba na ngoma ‘Kiba_100’ ambayo ni yake na Stamina (Rostam).

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW