Michezo

Ronaldo aweka wazi matarajio yake kuhusu tuzo za Ballon d’Or “Nisiposhinda ntakosa usingizi”

Ronaldo aweka wazi matarajio yake kuhusu tuzo za Ballon d'Or "Nisiposhinda ntakosa usingizi"

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno, Cristiano Ronaldo amefunguka na kusema mengi sana kuhusiana na nia pamoja na matarajio yake ikihusiana na malengo yake katika kuiwania tuzo kubwa kabisa duniani ya Ballon d’Or ambayo inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka huu December  3, mwaka 2018 ambayo itakuwa ni tuzo ya 53 tangu ianzishwe mwaka 1956.

Katika tu hii kubwa kabisa wanaongoza kutwaa ni wachezaji wawili tu duniani ambao ni yeye Cristiano Ronaldo akitwaa kwa nyakati 5 tofauti na anayefuatia ni Muargentina Lionel Messi akitwaa pia mara 5.

Wachezaji hawa wamekuwa katika mchuano mkubwa sana wa kila mmoja kutaka kuonesha yeye ni bora kuliko mwingine kwani hayo tunaendelea kuyaona katika mafanikio waliyonayo na hata kwenye kuwania tuzo mbalimbali.

Katika tuzo ambazo zinatarajiwa kutolewa mwezi desemba mwaka huu Ronaldo amefungula katika mahojiano aliyofanya na Kituo cha habari cha France Football na kusema ” Kama sitafanikiwa kushinda Ballon d’Or sitaweza kulala kwa kuwa nafanya kila juhudi uwanjani ili kufanikiwa kushinda tuzo ya 6 sio tu kwa kutegemea kura tu najituma ili nibakie kwenye kiwango changu kile kile kwa kujituma na kufanya kazi kwa juhudi zote kwenye mpira kwa zaidi ya masaa matatu hadi manne na nikitoka hapo naelekea gym kuweka mwili wangu sawa na kuupa utayari ambacho ni kitu cha msingi sana kitakacho ufanya mwili uwe na utayari wa kuendelea kupambana na kuendelea kubaki katika kiwango kile kile kwa mu mrefu,kiukweli ni ngumu tena ukiwa unafanya hiki kwa miaka mingi,ukiwa katika kiwango bora kwa zaidi ya miaka 12 bila kupata misukosuko lazima uweze kushinda tuzo kila mwaka hakuna mtu anayeweza kuamini hiki.

Ronaldo alimuuliza mtangazaji ” Unawajua wachezaji wangapi ambao wamefanikiwa kuwa katika ubora ule ule kwa zaidi ya miaka 10 ?, Unaweza kuwahesabu kwa kutumia vidole vyako vya mkono,au tunaweza kusema ni wawili tu, na ndio maana wanaendelea kuchuana na pia ndio maana mimi nimefanikiwa kufikia mafanikio haya, na ndio maana nina uchu na uchungu wa kuandika kitabu kitakachoelezea mchezaji bora zaidi duniani”.

Hayo ndio yalikuwa maneno ya Ronaldo katika mahojiano yake hayo ingawa tayari tuzo kubwa mbalimbali zimeshatolewa msimu huu zikiwemo tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa UEFA na mchezaji bora wa FIFA mwaka 2018 na katika tuzo hizo zote hakufanikiwa kushinda Ronaldo ingawa alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliokuwa wakiwania tuzo hizo, huku tuzo zote akishinda mchezaji wa klabu wa Real Madrid na taifa la Croatia Luca Madric.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents