Habari

Rwanda: Kiongozi wa upinzani atoroka gerezani kwa kuruka ukuta wenye ulinzi mkali 

Serikali ya Rwanda imeripoti kuwa makamu rais wa chama cha upinzani nchini humo cha  FDU-Inkingi,  Boniface Twagirimana ametoroka kutoka gereza la Mpanga International lililopo Nyanza District siku ya Jumapili.

Vyombo mbalimbali vya habari Rwanda vimeripoti hapojana kuwa serikali imethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kutoroka kwa kiongozi huyo wa ngazi za juu ndani ya chama cha upinzani.

Hilary Sengabo amesema kuwa Twagirimana na baadhi ya wafungwa wengine wameweza kutoroka kwenye gereza hilo baada ya kufanikiwa kuruka ukuta lakini uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea.

Hata hivyo wanachama wa chama hicho cha FDU wameshindwa kukubaliana na maelezo hayo huku wakilihusisha tukio hilo na maswala ya kisia nakuonyesha kuhofia maisha ya Twagirimana kuwa hatarinini.

Kwenye maelezo yaliyotolewa hapo jana siku ya Jumatatu FDU imekuwa ikiuliza inawezekanaje Twagirimana kutoroka kwenye gereza lenye ulinzi wa hali ya juu.

Mnamo Septemba mwaka 2017, Twagirimana na wanachama wengine nane wa chama cha FDU walikamatwa kwa makosa ya kuunda genge la kihalifu wa kutumia silaha dhidi ya Serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents