Technology

Sahau kuibiwa au simu yako kuishiwa chaji ukiwa na begi hili la kijanja

Kadri dunia inavyozidi kwenda utagundua kuwa watu wengi wanauhitaji mkubwa wa kubeba mizigo yao kutoka kwenye maeneo ya kazi ikiwemo vitendea kazi kama Laptop, Nguo za kazini kama sare, muda mwingine hata bidhaa ndogo ndogo kwa wale wafanyanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga ila changamoto kubwa inabaki kuwa ni usalama wa vitu vyao wanapokuwa kwenye usafiri wa umma

Mabegi ya mgongoni aina ya ‘Bobby’

Habari nzuri ni kwamba tayari changamoto hizo kwa sasa zimeshapata muarobaini kwani kampuni ya XD Designer imetengeneza mabegi maalumu ya mgongoni aina ya ‘Bobby’ ambayo yatakufanya uwe salama kwa asilimia 100 na uhakika wa kuwa hewani muda wote kwa kukuwezesha kuchaji simu yako

Mabegi hayo ya mgongoni aina ya ‘Bobby’ yana sehemu maalumu iliyofichwa zipu za kufungulia na sehemu hizo zinatofautiana kila begi kitu ambacho kwa haraka mwizi hawezi kuioana sehemu hiyo.

Unaweza ukajiuliza pia vipi kuhusu wale wezi wanaochana mabegi kwa kutumia vitu vyenye ncha kali, ukweli ni kwamba begi hilo limewekwa plastiki ngumu kwa ndani ambayo ni ngumu kutobolewa kwa urahisi.

Begi hilo pia lina sehemu maalumu ya kuchajia simu kwa kutumia USB ambapo mtumiaji atalichaji begi hilo kabla ya kuanza kutumia.

Sifa nyingine ni kwamba ukiwa na begi hilo hutaogopa kulowa na mvua kwani halipitishi maji, na lina sehemu maalumu ya kuweka Kadi zako za Benki, vitambulisho na simu yako ambapo hutahitaji kulivua wakati wa kuvitoa pale vinapohitajika.

Na kwa wale waendesha baiskeli hususani usiku begi hili limewekwa reflector kwa nyuma ambazo zitamlinda dhidi ya magari.

Mabegi yote ya kawaida ya mgongoni yanafunguka kwa nyuzi 30, lakini kwa begi hili la ‘Bobby’ litafunguka mfumo wa briefcase yaani nyuzi 30 hadi 180 kuendana na matumizi yako ili kumuwezesha mtumiaji kutoa vitu vyake kwa urahisi hata kama akiwa amelishikilia.

Begi hizo za aina ya Bobby zimetengenezwa na Kampuni ya XD Design ya nchini Ujerumani na lengo haswa likiwa ni kupunguza idadi ya matukio ya wizi kwenye sehemu za usafiri wa umma.

Bei elekezi iliyotajwa kupitia mtandao wa kampuni hiyo wa XD Design ni Euro 89.9, sawa na shilingi laki mbili na nusu za kitanzania na tayari unaweza ukanunua kwa njia ya mtandao. Tazama video hapa chini ujue kwa undani wa begi hilo janja la Bobby.

Hapa chini unaoneshwa jinsi mwizi anavyoshindwa kuiona, sehemu ya kuchaji na sifa nyingine nyingi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents