Habari

Said Comorian, TID na Ismail Wajieleza

TIDKile kinachosemwa kuhusiana na kuibiwa kwa wimbo ‘nyota yako’ wa msanii TID hatimae wahusika wanaswa live katika kituo cha redio cha Clouds Fm na kila mmoja alikuwa na yake ya kusema…

Mahojiano Clods FM


Kile kinachosemwa kuhusiana na kuibiwa kwa wimbo ‘nyota yako’ wa msanii TID hatimae wahusika wanaswa live katika kituo cha redio cha Clouds Fm na kila mmoja alikuwa na yake ya kusema japo hakuna muafaka uliofikiwa mpaka walipomaliza mahojiano hayo na mtangazaji DJ Fetty na B12.


“wimbo huu niliurekodi tangu mwaka 2002 tena niliuandikia studio na kabla ya kuurekodi tulianza kwa kurekodi demo na baadae nilikuja kuingiza sauti, nilikuwa na melody yangu na nilimuimbia Comorian kisha tukatengeneza biti, sasa nashangaa hata huyu Pasada alipotokea na tena nadiriki kusema kuna wapumbavu tu wameona Nyota inashine wanaleta zengwe kwani hakuna cha Pasada wala nini” alifoka TID.


Wakati huo huo msanii Ismail alikuwa na haya ya kusema kwani yeye wimbo wake khadija na wenyewe unashabihiana kisawasawa na wa TID na Pasada “wimbo wangu niliurekodi tangu mwaka 2003 lakini nilishangaa siku za hivi karibuni niliona video ya wimbo ‘nyota yako’ wa TID nikastuka sana nilipogundua unafanana na wangu nikamtumia ujumbe kumuuliza kuwa ameurekodia wapi? akaniambia kwa Said nikakaa kimya ila nachoweza kusema ni ngoma yangu na kanitengenezea Comorian, sasa prodyuza ndo anatakiwa aseme undani wa hili”


Ilipofika zamu ya Prodyuza Saidi Comorian alisema “kila mmoja ametengeneza wimbo kimpango wake na nasisitiza kuwa hizi nyimbo hazifanani kabisa, pia nadiriki kusema kuna watu wanaleta njama za kumdondosha TID kisanaa jambo ambalo sidhani kama kuna faida yoyote watakayopata.


Aliendelea kusema “nimefuatilia kiundani kabisa kuhusiana na huyu msanii ambapo ilivumishwa kuwa jina la wimbo wa msanii huyu Amour Pasada lina maana moja na wimbo wa TID yaani ‘Nyota yako’ kitu ambacho si cha ukweli, kwani katia kufuatilia nilikwenda mpaka ubalozi wa msumbiji ambapo niliwaelezea kuhusiana na msanii huyu kama wanamfahamu na wakadai hakuna msanii huyo nchini kwao, ila wanamjua huyo jamaa kuwa ni raia wa Angola na maana ya wimbo wake ni ‘mapenzi’ sasa iweje wazushe kuwa maana ya wimbo ni kama wa TID? Alihoji.


Kila mtu alikuwa na lake la kusema lakini mpaka mwisho wa mahojiano hayo hakuna suluhu iliyopatikana kwani kila aliyeulizwa kuwa nani anastahili kumiliki wimbo alisema mimi, lakini alipoulizwa Prodyuza Comorian alisema TID ana haki ya kuumiliki wimbo huo kwani ameshatoka na umeshamuweka juu.


Sikiliza nyimbo hizi kisha useme nani anastahili kulimiliki songi?


TID “Nyota Yako”
{play}tid_nyota_yako.mp3{/play}


Wimbo wa Pasada kutoka Angola
{play}pasada_nyota_yako.mp3{/play}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents