Habari

Sakata la mjusi aliyechukuliwa na Wajerumani enzi za ukoloni, laibuliwa Bungeni

Mjusi mkubwa wa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani ambaye anasadikika kuwa mkubwa kuliko wote duniani, ameibuia mjadala Bungeni, huku baadhi ya wabunge wakiibana Serikali wakitaka arejeshwe nchini.

Na Ramadhan Mbwaduke, Dodoma



Mjusi mkubwa wa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani ambaye anasadikika kuwa mkubwa kuliko wote duniani, ameibuia mjadala Bungeni, huku baadhi ya wabunge wakiibana Serikali wakitaka arejeshwe nchini.


Aliyeibua suala hilo bungeni ni Mbunge wa Viti Maalum, CCM, Mhe. Fatma Mikidadi aliyehoji sababu za kushindwa kumrejesha nchini mjusi huyo anayeliigizia taifa hilo fedha nyingi kwa utalii.


Ikaelezwa kuwa mjusi huyo aliyechukuliwa Lindi na Serikali ya Ujerumani enzi za ukoloni, ana urefu wa mita 22 na kimo cha mita 15 na hivyo kuwa mjusi mkubwa kuliko wote duniani hadi hivi sasa.


Kana kwamba hiyo haitoshi, mjusi huyo ikaelezwa kwamba ana mtoto mwenye kimo cha mita nne.


Suala la mjusi huyo kwa mara ya kwanza liliulizwa Bungeni mwaka 2000 na mbunge wa Peramiho Mhe. Jenesta Mhagama, lakini Serikali ikadai kuwa hakuna namna ya kumsafirisha na mahali pa kumuhifadhi nchini.


Akijibu swali hilo bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ya nchi, Mhe. Benard Membe alisema hivi sasa uwezekano wa kumrejesha mjusi huyo upo.


Akasema Serikali inafanya mazungumzo na Shirika la kimataifa la Unesco na Pan Afrika ili waweze kusaidia kumleta na ahifadhiwe nchini.


Wabunge walidai kuwa mjusi huyo ambaye hivi sasa amehifadhiwa katika Jiji la Berlin analiingizia taifa la Ujerumani fedha nyingi kwa vile watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanamiminika kwenda kumwangalia.


Wakasema endapo atarejeshwa nchini atakuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi, na hivyo kulinufaisha taifa kwa kuliingizia fedha nyingi za kigeni.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents